Kufuatia kuwepo kwa taarifa za kuuwawa Askari wa Jeshi la Polisi wanne huko Mbagala maeneo ya Mbande jana saa moja usiku, Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa linaendelea na uchunguzi ili kuweza kuwabaini wahalifu waliohusika na tukio hilo .
Akizungumza na Waandishi wa Habari jiji Dar es Salaam Kamishina Operesheni na Mafunzo CP Nsato Marijani Mssanzya aliwataja askari waliofariki katika tukio hilo ni E.5761 CPL Yahaya F.4660CPL Hatibu G.9524 PC TITO pamoja na PC Gastone .
”Wengine ambao ni raia walijeruhiwa katika tukio hilo ni pamoja Ally Chiponda, Aziz Yahaya ambao wote ni wakazi wa eneo la Mbande, katika tukio hilo majambazi hayo yalifanikiwa kupora silaha mbili aina ya SMG na risasi, hakuna pesa wala au mali ya benki iliyoharibiwa nidhairi wahalifu hawa walikuwa na kusudio moja tu la kuwashambulia askari polisi” alisema Kamishina Mssanzya.
Kamishina Mssanzya ameongeza kuwa baada ya tukio hilo kulikuwa na baadhi watu waliondika taarifa za kubeza na kukejeli mazoezi ya kawaida yanayofanywa na Jeshi la Polisi ambapo wengine waliandika ujumbe wa kushabikia tukio hilo la kuuwawa kwa askari polisi hao.
“Katika tukio hili la kushambuliwa kwa askari polisi kumekuwa na baadhi ya viongozi wa siasa ambao wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakiwahamasisha wafuasi wao wawashambulie askari polisi”aliongeza Nsato