Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / LEMA AKAMATWA NA POLISI

LEMA AKAMATWA NA POLISI

| No comment
Image result for godbless lema

Hali ya sintofahamu kwa upande wa siasa nchini imeendelea kujitokeza ambapo leo alfajiri Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Godless Lema amekamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake na anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya mahojiano.

Taarifa za kukamatwa kwa Lema zimethibitishwa na Meya wa jiji la Arusha Lazaro Calist lakini sababu za kukamatwa kwake hazikuwekwa wazi na hivyo kuwafanya watu wabaki na mshangao wasijue kilichotokea.

Jana napo makada kibao wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoani Kigoma walikamatwa wakituhumiwa kueneza vitendo vya uchochezi.