Mfumo wa vyama vingi ni hali ya kuwa na chama zaidi ya kimoja,katika nchi moja,Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa, ili kuleta maendeleo ya nchi, upinzani wa kisiasa sio kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani, kuwa na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii husika.
Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa uliorejeshwa katika katiba ya Tanzania mwaka 1992 ambapo kuna zaidi ya vyama 20 vikiongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndio Chama tawala.
Wingi wa Vyama hivyo ni kiashiria kikubwa kuwa nchi hii ina wanaharakati na wapenda mapinduzi wengi ambao kimsingi kama ukiwapa nafasi ya kuongea utajua ni wapi kama mtawala utakuwa umekosea kwakuwa kutoa fursa hiyo haimanishi utapinduliwa, hilo haliwezekani kwakuwa wewe ndio mwenye dola
Busara hiyo ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi kwaajili ya kukuza demokrasia na kuvitumia kama chachu ya maendeleo ukiacha mashinikizo kutoka nchi za kimagharibi, lakini Hayati Mwl. Nyerere aliiona na kuikubali na ndio maana hata katika mchakato wa kura za maoni asilimia 20% walikubali mfumo huo na asilimia 80% waliukataa ila kwakuwa mfumo huo unafaida kubwa katika nchi Mwalimu Nyerere aliupitisha.
Inawezekana ikawa ni hofu ya kutotaka kukosolewa ila kama serikali ya Rais Magufuli itawatumia wapinzani kama kioo itaweza kufanya tathmini zake kwa ufasaha kabisa badala ya kulitegemea baraza la mawaziri ambalo kimsingi sio rahisi na haliwezi kujikosoa,pia baraza hilo linaweza kufanya kazi kutokana na kasi ya Rais aliye madarakani.
source; mtembezi.com