Dully amesema amegundua mashabiki wake walikuwa wanamtaka Dully Sykes wa zamani.
“Kwangu mimi ‘Inde’ ni ukurasa mpya katika maisha yangu ya muziki, ni muda mrefu sijatoa ngoma ambayo imefanya vizuri kwa muda mfupi kama hii, kwa hiyo naweza kusema nimejifunza vingi, nimegundua mashabiki wa muziki wangu walikuwa wanamtaka Dully wa zamani, Dully wa kipindi kile,” alisema Dully Sykes.
Aliongeza, “Pia wazo la kumshirikisha Harmonize limeboresha sana hii kazi, nashukuru Mungu jicho langu lilikuwa zuri, mtu kama Harmonize ni msanii wa mbali sana, kwa hiyo mashabiki wategemee vitu vizuri sana kutoka kwangu,”
Video ya wimbo ‘Inde’ imefikisha views laki nane ndani ya wiki moja.