Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / AHADI YA JPM YA MILIONI 50 KILA KIJIJI YAIVA

AHADI YA JPM YA MILIONI 50 KILA KIJIJI YAIVA

| No comment
Image result for magufuli

BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), limesema mpango wa utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa Sh milioni 50 kwa kila kijiji na mitaa, maarufu kama Mabilioni ya Rais John Magufuli, umeiva.

Mpango huo uliobatizwa jina la Fedha za Mfuko wa Mzunguko, unalenga kukabiliana na tatizo la mitaji kwa ajili ya kuendesha shughuli za kiuchumi kwa wananchi wanaoishi maeneo ya mijini na vijijini.

pesa


pesaKatibu Mtendaji wa Baraza hilo, Beng’i Issa alisema Dar es Salaam jana kuwa fedha hizo zimelenga kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (Saccos) na vikundi vya kifedha vya kijamii vikiwemo Vicoba, kwa ajili ya kuanzisha au kuendeleza shughuli za kiuchumi.

Alisema hivi karibuni kumekuwa na taarifa kutoka sehemu mbalimbali nchini kuwa kuna baadhi ya taasisi na watu binafsi, wanawadanganya wananchi kuwa fedha hizo zitapitia kwenye taasisi zao na kuwataka wananchi kujisajili nao ili waweze kufaidika na fedha hizo, jambo ambalo si la kweli.

“Watu na taasisi hizo zinazowadanganya wananchi zimekuwa zikiwatoza viwango mbalimbali vya fedha kwa kile wanachodai ni ada ya usajili ili vikundi hivyo vya wananchi viweze kusajiliwa na kutambuliwa kuweza kufaidika na mamilioni hayo kwa kila kijiji,” alisema.