Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
AFANDE SELE AMGEUKIA BABU TALE
Imekuwa kawaida yake kumchana yeyote pale anapojisikia baada ya kuona mambo hayakwendi sawia, baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutangaza marufuku ya kuvuta sigara hadharani, uuzaji na matumizi ya shisha pamoja na biashara ya mashoga Afande Sele aliibuka na kusema “Sio jambo sahihi kwa mtu kama Mkuu wa Mkoa (Makonda) kutoka tu hadharani na kuongea vitu bila kufuata ushauri, sio sahihi” .
Afande Sele hakuishia hapo, Julai 15 mwaka huu kama kawaida yake ya kupovuka akamgeukia Mbunge wa Jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga baada ya kutaka sanamu la mnara wa askari pale Posta itolewe na kuwekwa sanamu ya Diamond Platnumz Afande akasema“Sikutegemea kuona mtu wa aina ile anakwenda kuongea na kufikia hatua ya kulidhalilisha jeshi kwa sababu mimi ni Mwanajeshi … sasa leo anatokea mbunge from no where, mtu ambaye ubunge wenyewe kaupata kama vile anakabidhiwa chupa ya chai hata haitingishwi na ikitingishwa inapasuka”.
Sasa yote tisa, kumi safari hii Afande Sele kaamua kumgeukia Babu Tale ambaye ni Meneja wa Tip Top Connection baada ya kukumbwa na masahibu ya kutozwa faini ya sh. milioni 250 aliyoamriwa na Mahakama Kuu ya Tanzania alipe baada ya kuvunja mkataba kati yake na Sheikh Mbonde wa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya sheikh huyo.

Kupitia mtandao wa Facebook Afande Sele amesema “Inawezekana faini ya shilingi milioni 250 alizoamriwa Babu Tale na Mahakama Kuu ya Tanzania amlipe yule Sheikh mwenye madai dhidi yake na nduguye ni ndogo sana kwao ukizingatia yeye Tale ndio meneja wa wamiliki wa Bongo Fleva kwa sasa. Lakini ukweli ni kwamba pesa yeyote inayotoka bila kuingia wala kutarajia inauma sana, … pole sana wakunyumba Babu Tale naamini haya ni mapito katika maisha na yatakwisha ingawa upande wa pili ni mafunzo kwetu wengine tunaojiona na kujiita wajanja wa mjini kuwa sheria ni msumeno na mahakama ni kama nyoka usimdharau kwa udogo wake wa umbo au umri, wote wanasumu na sumu humuua yeyote!”.