Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / TIJA YA MASHINDANO YA AIRTEL RAISING STAR KWA VIJANA.

TIJA YA MASHINDANO YA AIRTEL RAISING STAR KWA VIJANA.

| No comment



Michezo ina nafasi kubwa sana kwenye maisha ya binadamu hata katika haki za mtoto suala la haki ya kucheza limetambuliwa, na hii ni kutokana na umuhimu wake wa kiafya na kiakili, ndio maana wadau mbalimbali wamekuwa wakisisitiza suala la michezo kwa kukuza vipaji vya vijana.

Airtel Raising Star ni moja ya fursa ya kukuza vipaji kwa vijana wa Tanzania, ambapo kwa mwaka huu wamezindua msimu mwingine wa mashindano hayo, akizungumza katika uzinduzi huo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amewataka vijana kuitumia fursa hiyo ipasavyo kwani ndiyo njia ya wao kutimiza malengo yao, huku akimtolea mfano kijana Mbwana Samatta anae kipiga  katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ambapo amejizolea umaarufu na kuishi maisha mazuri kupitia mpira wa miguu.

Pia Rais huyo wa TFF Malinzi amewataka makocha wa timu za mpira wa miguu kutumia fursa hiyo na kuchagua wachezaji mahiri kwa fainali zijazo kwakuzingatia uwezo na tabia njema lakini siyo kwa kujuana, kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso amewashukuru wadau mbalimbali kwa kuwaunga mkono na kuviomba vilabu kutumia fursa hiyo kwa kupata wachezaji mahiri.

Mashindano hayo ya Airtel Raising Star kimkoa yanataraji kuendelea kuanzia Septemba 6 mpaka 11 kwa timu kutoka  Ilala, Temeke, Kinondoni, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Lindi, Zanzibar and Arusha, mpaka kufikia fainali.