Tuna uhakika muziki wa bongofleva una nguvu na unachezwa sana kwenye Radio na TV za Kenya lakini tukisikia kutoka kwa wenye media wenyewe ndio inakua fresh zaidi ndio maana nakukutanisha na Dj Hypnotic ambaye pia ni mkuu wa idara ya muziki Kiss FM Kenya.
Alikutana na millardayo.com na kuyasema yafuatayo >>> ‘Nitakutajia Wasanii ambao wana majina makubwa kwetu sasa hivi na wanachezwa sana, Ommy Dimpoz, Vanessa Mdee, Diamond anapendwa pia sana, Yamoto BAND ndio wako moto sana pia alafu Alikiba amerudi kwenye biashara naona anapendwa pia, sijawasahau Navy Kenzo wanachezwa sana pia