Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
MUSIC NEWZ
Aslay kaongea kwanini hayuko tena na Mwanamke aliyekua na ujauzito wake… natayari kashapewa majukumu ya umeneja.
Aslay kaongea kwanini hayuko tena na Mwanamke aliyekua na ujauzito wake… natayari kashapewa majukumu ya umeneja.
Aslay ni mwimbaji kutokea kundi la Yamoto BAND,
kilichofanya awepo kwenye hii post ni kauli yake ya kukanusha
kumtelekeza Mwanamke mwenye ujauzito wake baada ya kuishi nae kwa miezi
isiyozidi 6.
Aslay ambaye ana umri wa miaka 20 sasa hivi amesema ‘Baada
ya kuishi pamoja miezi sita tulizinguana ikabidi kila mtu ashike
hamsini zake, sisi vijana bwana mambo mengi… tukaangalia pia mimi bado
umri wa kukaa na Mwanamke na yeye akaona bado umri wake wa kukaa na
Mwanaume‘
Aslay na mzazi mwenzie
‘Sikuchukua uamuzi ila wote
ndio tulichukua uamuzi…. nilimuacha na ujauzito wangu na tayari
amejifungua mtoto wa kike ambaye ana kama mwezi mmoja na nusu, mwanangu
nimemuita Moza jina la marehemu mama yangu… na bado mpaka sasa tunaonana
hata hapa nimetoka kumuona mwanangu, hatujarudiana…. tunashirikiana tu
kama mtu na mzazi mwenzake‘ – Aslay
Kingine alichokiongea Aslay kwa sasa ni
kwamba amekabidhiwa majukumu mapya ya kuwa meneja, aliyemkabidhi ni
boss wake Mkubwa Fela kiongozi wa Mkubwa na Wanawe na sasa Aslay ni
meneja wa madada watano aliokabidhiwa miezi mitatu iliyopita na
watasikika very soon