‘Hii ni imani ambayo
nimeifikiria muda mrefu na nikajua lazima niifate, kila mtu ana kitu
ambacho anakiamini na kwangu naamini moto ndio kila kitu kwenye maisha,
kama maandiko yanavyosema Mungu ni moto ulao… naamini moto ndio mfumo
ambao hata Mungu anatokana na moto wenyewe‘ – Afande Sele
Kwenye sentensi ya pili Afande amesema ‘wakisema
Mungu hajulikani au Mungu hujui ni kitu gani hapo kwangu siwezi kuamini
kitu ambacho hakionekani kwa hiyo mimi naamini Mungu ni lile jua
linalowaka sababu ndio moto mkuu kuliko mioto yote, sasa kama Mungu ni moto ulao basi mimi napaswa niliwe na moto ule‘
‘Naamini
nikichomwa moto nitakua majivu, unaposema Mungu ni moto ulao inamaana
mimi moja kwa moja nitakua nimeliwa nimeingia ndani ya Mungu mwenyewe,
hata kesho nikifariki nikachomwa moto nikawa majivu, sipendi kufufuliwa
kwenye mazingira ya ubinaadamu tena sababu nimegundua ubinaadamu sio
kitu kizuri cha kujivunia‘
‘Japo binadamu wanaweza
kujivunia sababu ndio wanatengeneza Ndege, Magari na vitu vingine….
binadamu ndio kiume mbaya na muovu, msaliti, mnafiki, batili kuliko
kiumbe chochote katika ulimwengu, hata dunia yenyewe itamalizwa na
binadamu na sio kiumbe mwingine kwahiyo ili kuukana huu ubinadamu
sipaswi kuzikwa kwenye udongo, nikizikwa kwenye udongo manake
nitafufuliwa kama binadamu tena kitu ambacho sikitaki‘ – Hayo ni maneno ya Afande Sele msanii wa siku nyingi kwenye muziki wa bongofleva
Kwa kumalizia, Afande amesema ‘Mungu ninaemwamini
mimi ni moto na moto mkuu kuliko yote ni jua hata samaki anayeishi
chini ya bahari kabisa jua likiwaka asubuhi anatoa mgongo juu inamaana
anatoa heshima yake kwa Mungu, hiyo ndio imani yangu na wala
simlazimishi mtu mwingine yeyote aamini ninavyoamini mimi, hata familia
yangu na watoto wanajua baba akifa anatakiwa kuchomwa moto