KUHUSU KUMRUDIA MUNGU: Ni
kweli nimemrudia Mungu, ni maamuzi ambayo nimeyafanya mwenyewe baada ya
kuona vitu ni vilevile, dunia ni ileile na watu ni walewale ndio maana
nikaona sio vibaya nikaja na upande mwingine lakini hii haimaanishi
kwamba nitakua nafanya muziki wa Injini, nitaendelea na bongofleva
lakini muda mwingi nitautumia kanisani.
KUHUSU OMAN: ‘Ni
kweli nimekaa nchini Oman kwa zaidi ya miezi saba, nilikwenda kwa ajili
ya kufanya shows tu lakini nikapata tatizo kwenye VISA yangu, nilifanya
show za kuandaa mwenyewe ikafanikiwa mwanzoni lakini baadae hali
ikabadilika, nilikua na VISA ya miezi mitatu na nikaenda kwenye wiki za
mwisho’
‘Niliamua kuongeza VISA ili nibaki
Oman, nikatoa pesa mtu anilipie lakini kumbe hakwenda kulipia… nikakaa
nikawa nadaiwa pesa nyingi maana unachajiwa kwa siku pale unapoongeza
siku bila VISA, nikawa sitoki kwenda nje kutembea najifungia tu ndani
kwa miezi yote, nyumbani watu wakapanic napigiwa simu Mama kalazwa
hospitali sababu yangu…. ila baadae ndio nimekuja kupata pesa nikalipa
faini nikarudi Tanzania’
KUOLEWA NA MUARABU OMAN: ‘Waswahili
wanaoishi Oman hawapendani, hawapendi maendeleo ya watu, wana majungu
na wakawa wananitafutia ugomvi nigombane nipigane Polisi, kuhusu kuolewa
sijaolewa…. naapa sijaolewa, watu waliongea hivyo sababu nilikua na
boyfriend ambaye ni Mauarabu, mpaka sasa niko naye… tulikua karibu sana
ndio maana watu wakahisi nimeolewa nae‘
KUHUSU KUVUTA UNGA: ‘Nimekua
nikiona taarifa kwamba mimi natumia dawa za kulevya, nimesikitika sana
na ilitokea mara ya kwanza nilikua na msanii mwenzangu kwenye show sijui
anatumia hivyo vitu kwahiyo watu wakaona tumeshaungana ila sio kweli,
sijawahi hata kuona, najua dada yangu Ray C katokea huko na
aliyoyapitia’
KUHUSU KUVUTA BANGI: ‘Kweli
nilikua navuta bangi ila sasa hivi nimeshaacha baada ya kukalishwa
chini na familia hata boss, nilikua navuta bangi kutokea nilipotoa wimbo
wangu wa pili, nilivuta sababu ya stress…. kuna kipindi nilikua
natafuta hata mtu wa kunitungia nyimbo, show zilikata na marafiki zangu
walikimbia wote kipindi hicho nilipoandikwa kwamba navuta dawa za
kulevya‘
KUHUSU NYIMBO MPYA: ‘Nitatoa
single mpya kwenye wiki mbili hizi, tokea niko Muscat natumiwa msg
Rachel tumekumiss karibu…. namshukuru Mungu maana msanii kukaa nje kwa
miezi alafu watu wakawa wanakumiss hivyo ni bahati… watu wakae karibu tu
naachia single mpya soon’