Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
NEWZ
RAISI MAGUFULI AMTUMIA SALAMU ZA POLE MAMA TUNU PINDA.
RAISI MAGUFULI AMTUMIA SALAMU ZA POLE MAMA TUNU PINDA.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia
salamu za pole Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda aliyepatwa na
ajali ya gari, iliyotokea jana tarehe 08 Februari, 2016 akiwa safarini
kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la
Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro ambapo gari aliyokuwa
akisafiria Mama Tunu Pinda, ilipinduka baada ya kumgonga mwendesha
pikipiki aliyeingia ghafla barabarani.
Katika salamu hizo alizozituma kupitia
kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Rais
Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kutokea kwa ajali hiyo
na amemuombea Mama Pinda na Majeruhi wengine kupona haraka.
“Kupitia kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu
Pinda, naomba unifikishie pole nyingi kwa mkeo Mama Pinda kwa kuumia
katika ajali hii, na namuomba Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi wote ili
waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku” alisema Rais Magufuli.
Mama Tunu Pinda anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es salaam, na hali yake inaendelea vizuri.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
09 Februari, 2016