Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / PROF JAY AANZA NA MSAADA HUU JIMBONI KWAKE

PROF JAY AANZA NA MSAADA HUU JIMBONI KWAKE

| No comment

Mbunge wa Jimbo la Mikumi ambaye pia ni mwanamuziki wa Hip Hop Tanzania, Joseph ‘Prof Jay’ Haule, ametoa msaada wa chakula kwa wananchi waliokumbwa na hadha ya mafuriko kata ya Tindiga jimboni humo.prof-2-559x520

Katika mafuriko hayo, nyumba zaidi ya 600 zimeharibiwa na watu zaidi ya 5060 wameathirika na mafuriko hayo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, ameweka bayana kuwa ametoa tani 1 ya unga, maji lita 13000, Maharagwe, mafuta na dawa za mbu.

“Ndugu zetu wa kata ya Tindiga wamepata maafa ya mafuriko makubwa sana na mpaka sasa nyumba 600 zimeanguka, kaya zaidi ya 1300 zimeathirika sana na watu 5060 wanahitaji hifadhi,

Mimi kama mbunge nimepeleka tani moja ya unga, maji lita 13,000, Maharage, Mafuta ya kupikia, chumvi na dawa za mbu nakadhalika.

Bado ndugu zetu wanahitaji sana msaada zaidi ili waweze Kukabiliana na hali ngumu wanayokutana nayo…

Mahitaji ni Maji, Chakula, Mahema, chandarua na dawa za mbu