Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
NEWZ
PRO MBARAWA AIBUA WIZI WA MILION 700 ATCL .
PRO MBARAWA AIBUA WIZI WA MILION 700 ATCL .
DAR ES SALAAM
SERIKALI imebaini wizi wa takribani
shilingi Milioni 700 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupitia
kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo
visiwa vya Komoro.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na
wafanyakazi wa shirika hilo.

“Kufuatia upotevu huo Serikali imechukua hatua thabiti
ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi
ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi cha polisi kitengo cha
usalama mtandaoni ili kubaini mtandao mzima uliohusika ” alisema Prof.Mbarawa.
Aidha aliongeza kuwa kwa utaratibu wa
kawaida wa shirika hilo wakala anapewa ruhusa ya kuuza tiketi za ndege
kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na pale anapomaliza mauzo
anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa tena.
Prof.Mbarawa anasema kwa sasa wameanza
na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo la kulifufua kwa kununua
ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi na waadilifu.
“Siku mbili zilizopita
nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini mapungufu mengi
na hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika hii linarudi
kutenda kazi kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote wanaoenda kinyume
na maadili ya utumishi wa umma” alisema Prof.Mbarawa.
Vilevile aliongeza kuwa Serikali
imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kufanya
uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha
za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.