Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / PREZZO AWACHANA WASANII WA BONGO

PREZZO AWACHANA WASANII WA BONGO

| No comment
 

Kufuatia kukithiri kwa wimbi la wasanii wa nyumbani kufanya video zao nje ya nchi hususani Afrika Kusini na nje ya hapo, rapa mwenye makeke kutoka nchini Kenya maarufu kama Prezzo amewataka wasanii wa Afrika Mashariki kubadilika kimawazo na kuthamini waongozaji wa ndani.

 Akizungumzaia suala hilo katika kipindi cha Clouds E kinacho rushwa na Clouds TV msanii huyo amesema wasanii wamekuwa kama kondoo wakiona mmoja wao kafanya video nje nao wanaiga wakiamini watafanikiwa, hivyo amewataka wasanii hao kufanya kazi na waongozaji wa ndani kwani kuna sehemu nzuri (Locations), vitendea kazi ambavyo vitaifanya kazi kuwa bora na kuwavutia wasanii wengine wa nje kuja kuwekeza kwenye soko la ndani.

 Prezzo yupo nchini kikazi akiambatana na Menejimenti yake ambapo ameanza zoezi la upigaji picha wa video yake mpya chini ya muongozaji anaekuja kwa kasi Afrika Mashariki kutoka Wanene Film maarufu kama Hanscana.

Image result for hanscana director

vile vile msanii huyo ameweka bayana kuwa atafanya kolabo na baadhi ya wasanii wa Bongo akiwemo Mr Blue.

 Image result for mr blue