Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / Nina bajaji moja na bodaboda-Dayna

Nina bajaji moja na bodaboda-Dayna

| No comment

Msanii wa muziki Dayna Nyange amefunguka na kuweka wazi kuwa nje ya kazi yake ya muziki kwa sasa ameanzisha "kibiashara" ambacho kwa wiki kinaweza kumuingizia kipato fulani nje ya kazi yake ya muziki.

Dayna amesema hayo alipokuwa akipiga stori kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, lakini mbali na hilo amesema yeye kwa upande wake kampeni za siasa ambazo walikuwa wakizifanya hazikuweza kumuathiri kwani alikuwa anasimamia kile anachokiamini na wala si pesa zilizo mfanya kufanya kampeni.

Unajua sisi binadamu kila mtu ana uhuru wake kwa kile anachokiamini na kukisimamia, kwa upande wangu kampeni hazijaniathiri kwa lolote sababu toka kipindi kile mimi nilikuwa nawaambia ukweli watu kutokana na kile ambacho mimi naamini, hivyo watu walikuwa wanahoji sana kwenye mitandao na mimi nilitumia muda wangu kuwaelewesha juu ya kile nachokiamini mimi na uhuru nilionao mimi katika kitu nachokiamini" Amesema Dayna.

Lakini mbali na hilo ameshukuru kuona muziki wake unakua na kuona wasanii wengine wakubwa wanapenda kazi zake na kuonesha kufurahishwa na kile ambacho anakifanya.

"Unajua kama leo nimeona msanii Alicios amepost picha yangu na kusema kuwa anapenda sana muziki wangu hivyo nilipoona ujumbe huo kiukweli kabisa nilifurahi sanaa maana anaonesha ni jinsi gani anapenda kazi zangu" Alimalizia Dayna