Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
MUHONGO AANZA KUJIBU TUHUMA ZAKE ZOTE,IKIWEMO SAKATA LA ESCROW
MUHONGO AANZA KUJIBU TUHUMA ZAKE ZOTE,IKIWEMO SAKATA LA ESCROW
DODOMA
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo, amesema hajawahi kupokea rushwa kwa mtu yeyote wala
asilimia 10 ya wawekezaji wa miradi mbalimbali ya umeme nchini.
Aidha, ametaka kuachwa kuingizwa kwa
masuala ya siasa kwenye umeme, kwani umeme ni suala linalohitaji
utaalamu zaidi na si maneno

Alitoa kauli hizo juzi wakati akizungumza na wazalishaji wa umeme kwenye mkutano uliofanyika Mtera.
“Mimi hakuna mtu yeyote
dunia nzima aliyewahi kunipa rushwa, nia yangu ni kuhakikisha taifa
linapata umeme ikiwa ni pamoja na kuongeza wawekezaji, sihitaji hela ya
mtu,” alisema Profesa Muhongo.
Pia alisema baadhi ya mitandao ya
kijamii, imekuwa ikiripoti kuwa amewaita wazalishaji hao ili wamlipe
asilimia 10 ; na kusema jambo hilo si la kweli hata kidogo.
“Kwenye masuala mengine ya
mtandao ambayo hayana ukweli wowote muwe mnajitetea,” alisema Profesa
Muhongo. “Acheni kuingiza masuala ya siasa kwenye umeme,” alionya.