Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
MKURUGENZI WA MKOA AZICHARUKIA BAA NA KLABU HIZI ZA USIKU …!!
MKURUGENZI WA MKOA AZICHARUKIA BAA NA KLABU HIZI ZA USIKU …!!
SHINYANGA
MKURUGENZI Mtendaji wa Manispaa ya
Shinyanga, Lewis Kalinjuna amezifunga baadhi ya kumbi za starehe na baa
ya Dragoni iliyokuwa karibu na Shule ya Msingi Town kwa madai kuwa
zimekosa viwango vinavyotakiwa ikiwemo kukosa huduma za vyoo.
Licha ya changamoto hiyo, katika shule
hiyo ya msingi ndani ya madarasa kumekuwa mara kwa mara kukutwa na
kondomu ambazo zimekwisha tumika hali ambayo ni hatari kwa wanafunzi.

Akizungumza na waandishi wa habari
mjini hapa jana, mkurugenzi huyo alisema klabu za usiku za Bakurutu
maarufu Maduka Mengi, Lubaga Inn na Butiama zimefungwa mpaka
zitakapojirekebisha kwa kutengeneza huduma zinazotakiwa.
Kalinjuna alisema baa ya Dragon
imefungwa moja kwa moja kutoa huduma kwa sababu ya kutokukidhi viwango
hasa kukosa huduma za vyoo na kuwa karibu ya eneo la shule.
“Hizi baa za usiku zinazokesha
zimekuwa na changamoto nyingi hivi sasa ni suala la usafi kila maeneo
wao wanaendesha biashara hizo pasipokuwa na huduma za vyoo. Tumeamua
kuchukua hatua ya kuwasimamisha wasitoe huduma mpaka pale
watakapojirekebisha ila baa ya Dragon yenyewe tumeifungia moja kwa
moja,” alisema.
Mkurugenzi wa baa ya Dragon, Humprey
Godfrey alisema kitendo cha kufungiwa kimemsikitisha kwani wakati
akianza kufanya biashara hiyo alipewa leseni kutoka manispaa na kukagua
mandhari yake sasa imekuwaje leo kufungiwa moja kwa moja hilo suala
hawajatenda haki.
“Mimi nimeshangazwa na manispaa hii
ina maana hawakuona kipindi wanaponipatia leseni kuwa nipo karibu na
shule. Sasa nimeanza biashara wamekuja kunifungia kwa kueleza makosa
mengi hivyo hawajanitendea haki,” alilalama mkurugenzi huyo.