Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
NEWZ
MBARAWA ATOA TAMKO HILI KWA MAKANDARASI.
MBARAWA ATOA TAMKO HILI KWA MAKANDARASI.

Morokitaa blog inakuletea taarifa ya
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ambapo
amewataka Makandarasi waliosimamisha kazi za ujenzi wa barabara nchini
kuendelea na ujenzi baada ya Serikali kuanza kuwalipa madai yao.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi
wa barabara ya Magole-Turiani yenye urefu wa kilomita 48.6 Wilayani
Mvomero Mkoani Morogoro, Prof. Mbarawa amesema tayari Serikali
imeshalipa makandarasi mbalimbali nchini shilingi bilioni 400 na
itaendelea kufanya hivyo ili kumaliza madeni yao kwa haraka
“Hakikisheni mnarejea kazini na kuwapa
mikataba ya ajira wafanyakazi wenu katika kipindi cha wiki mbili kuanzia
sasa ili ujenzi wa barabara na madaraja ukamilike kwa mujibu wa mkataba
na hivyo kuondoa usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii”, amesema Prof
Mbarawa.
Profesa Mbarawa amemhakikishia mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation anayejenga
barabara ya Magole-Turiani kuwa tayari serikali imeshamlipa zaidi ya
kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya laki 735 na Shilingi za
kitanzania zaidi ya Milioni 795 hivyo ni wakati wa kukamilisha ujenzi huo hususan sehemu za madaraja kabla ya mvua za masika kuaanza.
