Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / Jux adai kufungiwa kwa video yake hakuwezi kumzuia kufanya kazi kubwa zaid

Jux adai kufungiwa kwa video yake hakuwezi kumzuia kufanya kazi kubwa zaid

| No comment

Msanii wa muziki wa R&B, Jux amesema kitendo cha kufungiwa kwa moja ya kazi yake ‘Uzuri Wako’ kwa madai alikiuka maadili hakuwezi kumzuia kufanya kazi kubwa zaidi kwa kuwa nia yake kwa sasa ni kwenda kimataifa zaidi.

Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Jux alisema ana shangaa kuona BASATA wanashindwa kuzuia video au kazi za nje ambazo mara nyingi zinakuwa na uchafu zaidi.

“Sijui ni kitu gani walikiona mpaka wakaifungia, japo wanasema maadili wakati kuna video za nje zinapigwa kwenye station za hapa ambazo zina vitu vibaya zaidi ya vyakwetu,” alisema Jux.

Aliongeza, “Kwahiyo mimi kwa muziki wangu haviwezi nizuia kwa sababu mimi nafanya muziki sio kuangalia Tanzania tu. Mimi muziki wangu nataka utanuke ndio maana nafanya video kubwa, nashoot video sehemu tofauti tofauti.Kwahiyo nikisema kwamba niwaangalia BASATA kwamba watafungia video, mimi sitaweza kumove on,”.

Jux kwa sasa anafanya vizuri na video ya wimbo One More Night.