Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
MUSIC
BASATA YAUFUNGIA WIMBO MPYA WA NEY WA MITEGO’SHIKA ADABU YAKO’
BASATA YAUFUNGIA WIMBO MPYA WA NEY WA MITEGO’SHIKA ADABU YAKO’
DAR ES SALAAM

Baraza la Sanaa nchini(BASATA)
limeufungia wimbo wa Ney wa mitego unaoitwa ‘shika adabu yako’ kutokana
na matumizi ya lugha chafu ndani ya wimbo huo.
Akiongea leo na kituo maarufu cha
redio, katibu mkuu mtendaji wa baraza hilo amesema ni wimbo ambao haufai
na anashindwa kumpima Ney ana akili za namna gani.
“Kitu ambacho hakifai
kwenye jamii sio mpaka litolewe tamko kwamba wimbo umefungiwa, ni wimbo
ambao haufai hata wanajamii wameona haufai, nadhani mtu mwenye akili
timamu kiujumla anajua, najua kwenye media hauwezi kupigwa”
Wimbo huo mpya kutoka kwa Ney wa Mitego ulisika Live kwa mara ya kwanza kupitia kipindi cha XXL.
Katika wimbo huo uitwao ‘Shika Adabu
Yako’, Ney amewaumbua kwa kuwataja majina wasanii na watu maarufu nchini
akianika ubovu wa matendo yao na kuwataka wabadilike.
Pia katika wimbo amewaimba baraza la
Sanaa la Taifa(BASATA) kwa kuwaita ni msumeno usiokata na kazi yao ni
kufungia nyimbo ilhali hawajui shida wanayopata na kama wangekuwa watoto
angewachumia fimbo.
Pia hakumuacha nyuma Magufuli na
serikali yake kwa kusema amezoea wasanii ndio watu wanapenda umaarufu
lakini safari hii ligi ya umaarufu ipo kwenye serikali kwa kila kiongozi
kuwa na mwandishi kisha kushindana magazetini.