Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
NEWZ
AFISA MIPANGO ACT WAZALENDO APIGWA CHINI
AFISA MIPANGO ACT WAZALENDO APIGWA CHINI
.
Chama
cha ACT Wazalendo kimemsimamisha uanachama Ofisa Mipango wake, Ali
Makame Issa kwa madai ya kukiuka maadili ya chama hicho.
Hata hivyo, Issa alisema jana kuwa hajapokea taarifa yoyote kutoka katika chama hicho.
Hatua hiyo dhidi ya kiongozi huyo
mwandamizi ndani ya ACT, imekuja baada ya chama hicho kudai kuwa
alishirikiana na aliyekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar, Khamis Iddi
Lila kuwahujumu.
Awali, Lila alisimamishwa uanachama kwa
madai ya kutoa misimamo ya kushiriki uchaguzi wa marudio uliotangazwa na
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha.
Barua ya ACT, iliyosainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Juma Said Sanani imesema: “Kamati
maalumu ya Zanzibar imekusimamisha rasmi uanachama kwa mujibu wa katiba
ya ACT Ibara ya 11 (2) kuanzia leo Februari 19, 2016, kwa ukiukwaji
mkubwa wa katiba Ibara ya 7 (3)(5)(9) Ibara ya 10 (2)(c) (d), Ibara ya
22 (1) (2) (4).”
Barua hiyo inabainisha kuwa mwanachama huyo amekiuka kanuni na maadili pamoja na kukidhalilisha chama.
“Huku ni
kukiingiza chama katika mgogoro kwa kuandika barua ya kushiriki
uchaguzi wa marudio na kuhudhuria katika kikao cha Tume ya Uchaguzi
Februari 17 ukijua kuwa chama kimeshapeleka barua Febuari 9 ya
kutoshiriki uchaguzi,” inaeleza.
Vyama vilivyowachukulia hatua viongozi
wake kwa madai ya kukiuka kanuni ni Sauti ya Umma (SAU), kilichomfukuza
aliyekuwa mgombea wake wa urais wa Zanzibar, Issa Mohamed Zonga, huku
Alliance for Democratic Changes (ADC) kikimfukuza aliyekuwa mlezi wake,
Hamad Rashid Mohamed.