Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / TATOO YENYE JINA LA WEMA ALIYOICHORA KAJALA BAADA YA KUACHIWA HURU

TATOO YENYE JINA LA WEMA ALIYOICHORA KAJALA BAADA YA KUACHIWA HURU

| No comment


Baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya shilingi milioni 13 bila kusita ili kumuwezesha kutokufungwa miaka 7 jela. mara baada ya kutoka Kajala aliamua kuchora tatoo iliyoandikwa Wema mgongoni kwake..baada ya kuulizwa swali la kwanini ameamua kuchukua uamuzi huo

"kusema ukweli namshukuru sana Wema kwa alichonifanyia, najua maisha ya kule we acha tu, hata kama kuna chochote kitakachotokea nitaendelea kumkumbuka kwa yote aliyonifanyia na ndio maana nimeamua kuchora tatoo hii kwasababu nitamkumbuka milele." amesema kajala

Baada ya kutoka sasa hivi kajala yuko mbioni kutengeneza movie inayoitwa Pincess Sasha" chini ya kampuni ya Wema"endless fame". 

swali lilikuja kwa wema, anafanya movie na Kajala ili kurudisha pesa zake alizomlipia kama faini?

"ukweli mi sijafikiria hivyon na siwezi kufanya hivyo, nimefanya hivyo kwasababu kajala ni rafiki yangu, na sio kwamba sitamlipa akifanya movie hiyo hapana, nitamlipa kama kawaida." amesema Wema.
Kajala  ataigiza kama muhusika mkuu kwenye movie hiyo ambayo wako mbioni kuitengeneza